-->

Wolper Ageuka Kungwi

Msanii wa filamu bongo ambaye sasa amegeukia ujasiriamli, Jackline Wolper, amewapa somo mabinti na kuwafunda juu ya kujishughulisha ili kujipatia kipato chao, na hatimaye waweze kuheshimika.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Jackline Wolper amesema ni wakati sasa mabinti kuacha kutegemea pesa wanazopewa na wanaume, na badala yake wajishughulishe ili kutengeneza pesa yako mwenyewe. “Wadogo zangu wa kike 2018 mi ntaendelea kuwatia hasira, na kuendelea kuwaambia kwamba hela ya mwanaume sio ya kwako, ukishachukua hela ya mwanaume fanya kitu chako, iwe hela yako, usikubali kunyanyasika, kwa hela ya mtu, kwa hiyo wadogo zangu nitaendelea kuwaisipire ili mfanye kazi ili utambe na hela yako, usitambe kwa hela ya kuhongwa”, amesema Wolper.

Hivi sasa Wolper anamiliki biashara yake ya mavazi ambayo ana buni na kushona mwenyewe, ambayo aliwahi kusikika akisema inamuingizia pesa nyingi ingawa watu wengi wakimdharau kwa kumuita ‘fundi cherehani’.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364