-->

Baada ya Jimmy Mafufu Kushindwana na Jason Stathan Amvaa Niva

Riyama akiwa na Mafufu katika filamu ya Ishakua soo

Riyama akiwa na Mafufu katika filamu ya Ishakua soo

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahilihood Jimmy Mafufu amemwangukia msanii wa filamu Bongo Zubery Mohamed ‘Niva’ kwa kumshirikisha katika filamu ya Ishakua soo sinema ambayo ipo njia kutoka tarehe 15.February .2016 awali msanii huyo alikuwa na mpango wa kumshirikisha msanii mkubwa kutoka nchini Marekani Jason Statham katika filamu hiyo ambayo ni filamu ya kipekee kwa mujibu wa Jimmy Mafufu.

“Nilisema toka awali kuwa nataka kuwatumia wasanii kutoka nje kama vile Jason Statham lakini bei yake alikuwa anataka kunichaji kama Producer wa Hollywood kumbe mimi ni mtayarishaji wa Bongo ambaye filamu zetu zina bajeti ndogo, lakini nikiri kwamba Kijana wangu Niva kaitendea haki Ishakua Soo,”anasema Jimmy.

Jimmy Mafufu akiwa na Niva katika ‘scene’ ya filamu ya Ishakua soo

Jimmy Mafufu akiwa na Niva katika ‘scene’ ya filamu ya Ishakua soo

Filamu ya Ishakua soo imeshirikisha wasanii nyota kama vile mwanadada Riyama Ally, Niva, Asha Boko, Joseph Onyango, na wasanii wengine kibao wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu  na inasambazwa na Steps Entertainment nchi nzima katika kuwajengea wasanii maslahi hakikisha unanunua filamu halisi.

FC

Subscribe kwenye channel ya Bongo Movies TV kwenye Youtube ujionee video nyingi zaidi za Bongo Movies

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364