-->

Naepuka Kutumika Bila Faida – Lulu

Staa wa filamu Diana Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kama unamtaka kumshirikisha katika filamu yako, andaa milioni 15 kwani anaogopa kuendelea kutumika bila faida.

LULU53

Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV Jumapili hii, Lulu alisema tayari alishatengeneza jina kwa miaka mingi na sasa anahitaji pesa.

“Kufanya filamu kwa milioni 15 sio hela nyingi, watu wanaongea tu kwa sababu hawajui nini kipo ndani yake. Mimi nikipewa milioni 15, mavazi pamoja na kila kitu najitegemea.” Alisema Lulu

Aliongeza, “Kwa hii milioni 15 ni kweli kuna faida, faida moja ni kwamba naepuka kutumika bila faida, kwamba mtu unakuwa na jina sawa, umefanya movie hii, umefanya movie hii nini unacho?. Mwisho wa siku tunajikuta tunaanza kufanya vitu vingine ili kumaintain ile status yako kwa sababu umeshatengeneza jina na unahitaji kulimaintain.” alimalizia Lulu.

Bongo5.com

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364