-->

BASATA Waishikisha Adabu ‘Shika Adabu Yako’

Baraza la sanaa la Taifa BASATA limeufungia rasmi wimbo wa msanii Ney wa Mitego ‘Shika adabu yako’, ambao umeleta gumzo kubwa na mtafaruku kwa wasanii wengine na BASATA.

nay62

BASATA imetoa taarifa hiyo kwenye ukurusa wake wa twitter, na kuelezea kuwa wameamua kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili na uchochezi.

“BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, uchochezi”, waliandika BASATA.

Pia BASATA imesema itamchukulia hatua za kisheria msanii huyo na kumtaka kutoutangaza wimbo huo.

“BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha kuutangaza wimbo huo katika media, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa,

Pamoja na hayo BASATA imesema wasanii wengi wanatumia muda mwingi kubuni na kutengeneza kazi nzuri, lakini kuna wachache ambao wanaharibu, hivyo hawatawafumbia macho watu hao.

“Wasanii wengi wanafanya kazi zao vizuri, kwa kubuni kazi zenye ubora na zinazolipa sifa taifa, wachache wanaharibu, wanapakaa matope , BASATA halitavumilia hawa ‘wasanii’ wachache wanaotaka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni, wasio na staha,wa kudharaulika”, ilisema BASATA.

Kwa mujibu wa sheria kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa Baraza nguvu ya kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha kufanya majukumu yake kwa faida na ustawi wataifa.

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364