-->

Bifu la Diamond, Blue, Afande Sele Aibuka

LILE bifu la kugombania jina la Simba ambalo linawahusisha wasanii nyota wa Bongo Fleva, Henry Samir ‘Mr Blue’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’ lime­muibua mkongwe Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ ambaye alikuwa kwenye mishe za siasa.

Simba-1

Afande Sele maarufu Mfalme wa Rymes, aliyeku­wa akigombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Mjini, amesema yeye ndiye mwanzilishi wa jina hilo miaka mingi iliyopita.

“Hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuambia, mimi ndiye Simba Dume. Mwaka 2008 nilifanya wimbo na P Funk Majani, unaitwa Simba Dume na nikaanza kutumia hilo kutokea hapo, nawashauri waachane na mabifu yasiyo na maana.

“Ni bora wote watatu tukutane, tufanye kolabo, kila mmoja aelezee usimba wake kwenye mashairi, naamini itabamba na itakuwa na maana na faida kwa kila mmoja na mashabiki wetu,” alidadavua Afande Sele.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364