Idris Ajipoza kwa Lulu
Siku chache baada ya taarifa za kutoka kwa mimba ya mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshot’ 2014, Idris Sultan amebambwa kiwanja akijipoza machungu na staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Amani limenasa tukio.
Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilijiri wikiendi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Sky-Night Life uliopo Masaki jijini Dar ambapo wawili hao walikuwa wakijiachia wakati wa shoo ya Love Posion iliyokuwa imeandaliwa mahususi kwa msanii wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ katika kukamilisha shamrashamra za Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day).
Wakiwa ndani ya ‘kiota’ hicho wakila bata, wawili hao walibambwa uso kwa uso na kamera yetu ambapo mwanzo walijifanya hawafahamiani huku Idris akisimama kando ya sehemu aliyokuwepo Lulu na ndugu zake.
Mambo yalianza kubadilika baada ya Belle 9 kupanda jukwaani ambapo Idris ambaye inasemekana alilia kama mtoto baada ya kusikia mimba ya Wema imetoka, alishuhudiwa akimsogelea Lulu aliyekuwa meza moja na mwigizaji Rose Peter ‘Muna’ na Mtangazaji wa CloudsTV, Casto Dickson.
Baada ya kumsogelea, Idris alimsalimia Muna kisha akamkumbatia Lulu kwa takriban dakika mbili na kuanzia hapo ndipo mambo yakawa ‘shatashata’ huku wakipiga stori ndipo kamera yetu ikawageukia na kuanza ‘kuwafotoa’ hatua kwa hatua.
Akiwa ameketi ‘veri klozi’ na Lulu, Idris alionekana kuwa mwenye tabasamu ‘baab’kubwa’ ambapo wakati wote vilisikika vicheko, ikiwemo kunong’onezana mara kadhaa, jambo lililosababisha baadhi ya wadau kuhojiana kama Idris amehamishia majeshi kwa Lulu au la.
“Ebwana eeh, ujue mimi kama sijaelewa uwepo wa Lulu na Idris hasa kinachonifanya kushangaa ni namna ambavyo wawili hawa wanaongea tena kwa kunon-g’onezana wakati kama maongezi yao yasingekuwa na tatizo si wangeongea tu kama walivyokuwa wakisalimiana kwa sauti na wenzao wakawa wanasikia?” alihoji mmoja wa wadau hao.
Baadaye Idris alionekana akijipenyeza kuondoka ukumbini hapo ambapo dakika chache Lulu naye alimfuata akiwa na wenzake.
Hata hivyo, kila mmoja alipoulizwa kulikoni kama kuna kinachoendelea kati yao, hawakutoa ushirikiano huku nyumbani kwa Wema, Ununio, Tegeta jijini Dar, kukidaiwa kuwa kama kuna msiba kufuatia tukio la kutoka kwa mimba ambalo bado ni gumzo.
Chanzo:GPL