-->

Fella, Tale Kumrudisha Upya Chid Benz

MKURUGENZI wa kundi la Wanaume Family na Yamoto bendi, Saidi Fella maarufu Mkubwa Fella, amesema yeye na meneja wa msanii, Diamond Platnumz, Babu Tale, wameamua kumsaidia mkali wa rapu, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, arudi katika sanaa yake na si kujiunga na kundi lolote.

chid45

Chid Benz

Fella alisema msanii huyo kwa sasa wamemwanzishia mazoezi maalumu ya kumwezesha kurudisha mwili wake na pumzi ili aweze kurudisha makali yake katika uimbaji bila kuchoka.

“Chid Benzi hawezi kujiunga na Wasafi kwa sasa mimi na Babu Tale tumekubaliana tumsaidie yeye kama yeye na si kujiunga na kundi lolote lakini kama anataka kujiunga na lebo yoyote hilo litakuwa la kwake,” alifafanua Mkubwa Fella.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364