-->

Filamu ya Kiboko Kabisa Yaifunika Filamu za Mwaka Huu Zote!

ILE filamu kubwa ya Kiboko kabisa kila kona ni Kiboko kabisa inakimbiza Sokoni kila ukikutana na mpenzi wa filamu anasema Kiboko kabisa kwa utafiti uliofanywa na FC unaonyesha kuwa filamu hiyo imezifunika sinema zote toka kuanza kwa mwaka huu sambamba na filamu ya Chungu cha Tatu iliyotoka kabla ya Kiboko Kabisa.

KIBOKO45

Kijana mmoja muuzaji maarufu wa filamu za Kibongo amesema kuwa sinema za Nisha’s Film Productions zinakuwa na kawaida ya kufanya vizuri kwani kila zitokapo lazima zikimbize sokoni kutokana na hadithi zake sambamba na wasanii wanaoshiriki.

“Mjomba hapa unaponiona narudi Kariakoo kuchukua mzigo Kiboko Kabisa filamu hiyo imeifunika sinema ya Chungu Cha Tatu, watu wanaiulizia sana ukichukua copy chache unapata usumbufu, si unajua kazi za Nishabebee tena?,”anasema kijana aliyejitambulisha kwa jina la Omary Chakasa

Chinga huyo amesema kuwa wateja wake wamemwelewa sana Nisha , King Majuto, Mzee Jengua , Ben Blanco na wasanii waliocheza kama Madenti hivyo toka awali wamekuwa wakisumbuliwa kabla ya filamu kutoka kwani kila mara walikuwa wakiagizwa nakala za filamu ya Kiboko Kabisa .

Filamu ya Kiboko kabisa inapatikana katika maduka yote ya Steps Entertainment nchi nzima na maduka yote yauzayo kazi za kibongo nunua nakala halisi wala usihangaike na Dvd za buku buku ni mbovu utapoteza mkwanja wako bure ulie baadae .

Fc

Subscribe kwenye channel ya Bongo Movies TV kwenye Youtube ujionee video nyingi zaidi za Bongo Movies

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364