-->

Huenda Alikiba Akatoa Ngoma Muda Wowote

Msanii wa Bongo Flava, Alikiba huenda akatoa ngoma mpya muda wowote.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma Seduce Me katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika ujumbe ambao kwa kiasi fulani unahashiria ujio wa ngoma mpya.

Ujumbe huo ambao ulilenga kumpongeza msanii mwenzake, Abby Skillz kwa kufunga ndoa uliishia kwa kudokeza hilo.

Hongera Mkongwe nakutakia Kheri Na mafanikio Katika Ndoa Yako
Na ngoma Mpya Inafuata
#SapportedByKiba
#KingKiba

Hata hivyo haijaeleweka iwapo ngoma hiyo itakuwa ya Abby Skillz pekee kwani amekuwa akifanya kazi na Alikiba kupitia King’s Music. Ikumbukwe wawili hawa walishatoa wimbo pamoja mwaka jana ‘Averina’ ambao Mr. Blue alishirikishwa pia.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364