Kisa Gauni, Wema Ashindwa Kuhudhuria Uzinduzi Wa Idriss
Diva anayebamba kunako tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuhudhuria uzinduzi wa viatu vya x- wake, Idriss Sultan, kutokana na fundi kumharibia nguo yake.
Wema ameonyesha kusikitishwa kwa kitendo hiko, hasa ukizingatia kwamba Idriss alimsapoti kwa asilimia kubwa katika uzinduzi wa filamu yake ya Heaven Sent. Na kupitia ukurasa wake wa Instagram, amemuomba radhi na kumuelezea kilichotokea.
“Siku zote tunavutia sana kwenye red kapeti, nimejisikia vibaya sana kwa kushindwa kuhudhuria katika uzinduzi wako jana usiku, ndiyo maana nimeshawishika kusema samahani, nimehuzunika sana.
“Ni kweli wewe ulikuja kwenye uzinduzi wa filamu yangu na ukanisapoti sana, hamuwezi amini jana mpaka na saluni nimeenda, nilikuwa tayari kwa kuja, ila kilichotokea, Dah! Elisha kaniharibia nguo yangu, nimelia kama mtoto, sijui imekuwaje, maana Elisha hajawahi kabisa kunizingua kwenye nguo zangu ila ndiyo bahati mbaya sikuwa na nguo nyingine ya kuvaa na muda ulikuwa umeshakwenda, maduka ya nguo yote yalikuwa yamefungwa. Wenyewe mliona Idriss alivyopendeza halafu mimi ndiyo niende nikiwa sijapendeza.
“Labda hili siyo muhimu kwenu, lakini muonekano mzuri kwenye red kapeti ni muhimu jamani, yaani sijui hata niseme nini, kwa jinsi alivyonisapoti , inaumiza sana kwamba nimeshindwa kuwepo jana.
“Naombeni mnisaidie kumuelewesha japo anielewe maana najua kama binadamu, lazima amejisikia vibaya sana,” ameandika Wema.
NA ISRI MOHAMED/GPL