-->

Mguu Wamzima Stara Kisiasa

Msanii mkongwe wa muziki Stara Thomas, amesema kuwa aliyokuwa amepata katika mguu imezima ndoto yake ya kuingia katika siasa katika kipindi cha uchaguzi kilichopita.

STARA

Stara aliyekuwa na mpango wa kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum huko Mwanza ambapo ni nyumbani kwao, katika mahojiano aliyofanya na Planet Bongo ameeleza kuwa, harakati za kisiasa zinahitaji mtu kuwa fiti ili kuweza kuhimili mikiki na mizunguko ya kujinadi, kitu ambacho hakikuwezekana kutokana na hali aliyokuwa nayo.

Nyota huyo amesema kuwa, mpango wake huo bado upo akiwa amelenga kujikita kwa nguvu zote mwaka 2020 wakati awamu ya uongozi uliopo sasa utakapomaliza muda wake madarakani.

Chanzo:EATV.TV

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364