Nataka Niache Kula Monde-Juma Nature
Msanii mkongwe katika tasnia ya bongo fleva Juma Kassim Nature (Kiroboto) amefunguka na kusema ameachana na mambo mengi ya ajabu ajabu na starehe na kusema anataka kuachana na mambo hayo kwani uhuni ataki tena.
Juma Nature akipiga stori katika kipindi cha Planet Bongo ya EATV alisema ameweza kuachana na mambo mengi ambayo kwa jamii yanaonekana ni mambo ya kihuni lakini mpaka sasa bado hajafanikiwa kuacha monde (Pombe).
“Unajua kwa sasa nimeachana na mambo mengi yale ya kihuni huni ila nahangaika saizi kuachana na monde tu kwani hiyo mpaka saizi bado napiga ila nataka kuiblock pia” Alisema Juma Nature
katika hatua nyingine mkali huyo ameelezea kuwa katika sanaa na muziki hakuna uzee kwani anaamini anaweza kuandaa show ya wakongwe kwenye muziki na watu wakatokea wengi sababu wanapenda muziki.
Eatv.tv