Nay wa Mitego Afunguka Kuhusu Siwema, Mzazi Mwenzie
Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kuzungumzia nini kinaendelea baada ya kutangaza kumsaidia aliyekuwa mpenzi wake Siwema ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kumtukana shabiki kwenye mtandao wa kijamii.
Nay na Siwema walifanikiwa kukaa kwenye uhusiano kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata mtoto ambaye walimpa jina la Curtis kabla hawajatengana.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego alisema tayari ameshatuma wanasheria wake na wanaendelea kulishughulikia suala hilo kwa ukaribu zaidi.
“Nashukuru Mungu mambo bado yanaenda vizuri, wanasheria wangu wanalishughulikia hili suala kwa ukaribu zaidi. Naamini tunaweza kumsaidia. Lakini sio nataka kumsaidia kwa sababu ni mpenzi wangu, tayari tulishaachana na hatuwezi kurudiana,” alisema.
Aliongeza, “Mimi sasa hivi nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine, pia na yeye bila shaka alikuwa kwenye mahusiano. Kwa hiyo mimi nimemsaidia kibinadamu zaidi, kama alinikosea tayari yalishapita, hakuna aliyemkamilifu.”
Bongo5