-->

Nay wa Mitego auelezea mkasa wa mwanae Curtis na mzazi mwenzie Siwema

Rapa Nay wa Mitego amedai alimnyang’anya ex wake Siwema mtoto wao Curtis baada ya kile alichodai mwanadada huyo kuendekeza starehe za club pamoja na kusafiri nje ya mkoa kwa zaidi ya wiki mbili huku akiwa amemuacha mtoto nyumbani.

nay

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay alisema aliamua kumhifadhi lakini huu ni wakati wake sahihi wa kuweka wazi kila kitu ili wengine wajifunze.

“Sio kwamba sikuwa na matatizo kwa mzazi mwenzangu ila yake yalikuwa yamezidi na nilikuwa napata taarifa nyingi,” alisema Nay.

“Nilikuwa naambiwa mambo mengi lakini ilifika time mwenye nyumba wa nyumba ambayo alikuwa anakaa yeye alikuwa ananipa taarifa nyingi na kuniambia ‘mimi namwonea huruma huyo mtoto, sitaki kuwaachanisha kama mama yako yupo kwanini usiongee na huyu mwanamke wako ukamchukua huyu mtoto!’

Wakati anaanza kufanya mambo yake alikuwa anajificha lakini ilipofika time akawa anajiachia tu, kiasi kwamba mimi nikawa napata taarifa. Kuna washkaji wangu wakawa wananipigia simu wewe huyu mpenzi wako si analea mbona tuko naye club? Mimi nikimpigia anarukaruka lakini ukweli ulikuwa unaonekana” alifafanua.

Aliongeza, “Mimi nilikuwa namwambia huyo mtoto bado mdogo kama unahisi mimi na wewe penzi letu limefika tamati hebu ngoja huyu mtoto akue. Baada ya muda nikasikia unajua gari zangu zote zina plate namba 966, kuna gari ambayo mimi nilikuwa naitumia nikampa ilikuwa Mark X. Hiyo gari ikawa imeonekana sehemu za Geita. Kuna mtu akanipigia kuniuliza kama nipo Geita nikamwambia no, hiyo gari ni yangu lakini sipo huko hebu nipigie picha hiyo gari, akapiga picha akanitumia ilikuwa car wash.

Nikamwambia ni kweli hiyo gari ni yangu ikabidi nimpigie simu Mama ‘Curtis’ akaniambia nipo nyumbani, nikamwambia no haupo nyumbani. Nikamwambia kama upo nyumbani naomba nimsikie mtoto kwa bahati mbaya au nzuri kipindi kile alikuwa amefungua duka la nguo akasema nipo dukani na mtoto yupo nyumbani. Kumbe yupo Geita ana wiki ya pili na hajui mtoto anaendeleaje!. Watu wamezungumza sana kuhusu hili suala ila this time ngoja nizungumze ili kila mtu ajue.”

“Mwisho wa siku nikagundua ni kweli alikuwa two weeks bahati mbaya msichana wa kazi aliyekuwa nyumbani kwangu baada ya kuzinguana na msichana wake aliyekuwa anakaa naye pale, ikabidi msichana wangu mimi atoke nyumbani kwangu aende Mwanza kwa ajili ya kukaa na mwanangu. Kwahiyo asingeweza kunificha chochote.

Kwahiyo nilikuwa napata taarifa kila sehemu. Siku moja nikaona mtoto wangu ataharibika, kuna mtu akanipigia simu akaniambia leo ilikuwa saa kumi alfajiri naambiwa mpenzi wako yupo na mwanaume nilikuwa natoka studio nikaamua kwenda kumchukua na toka nimemchukua mpaka leo hajawahi kupiga simu.

Chanzo:Bongo5.com

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364