-->

Nay wa Mitego: Kuongea Kwangu Ukweli Kunanisababishia Nisiwe na Marafiki

Nay Wa Mitego amesema ngoma zake zenye mashairi yanayowahusu baadhi ya wasanii zimemfanya akose marafiki na baadhi yao ambao alikuwa nao karibu kumtenga.

nay987

‘’Ilishawahi kutokea nilipotoa ngoma yangu ya ‘Salamu Zao’ kuna baadhi ya washikaji zangu ambao nilikuwa nao karibu walinikimbia wakajua chochote kinaweza kutokea,nilipotoa nyimbo zingine haikuwa hivyo,ila nilipoa ngoma yangu mpya baadhi yao wamenikimbia na kunitenga tena hasa baada ya wasanii kuongea sana kuhusu hiyo ngoma,’’Nay.

‘Lakini sijali mtu akinitenga kwa kuwa nimeongea ukweli,ila nitaumia sana kama nikitengwa na mashabiki wangu, sijawahi kupata vikwazo kama ninavyovipata hivi sasa,najua kwa wasanii hiki ninachoimba kinaonekana si sawa kwao, ila kwa mashabiki wangu ni sawa’,Nay.

Cloudsfm.com

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364