-->

Ni Mvutano Kati ya Ray na Batuli Kuhusu Madai ya Pesa

batul22

Kutoka Mtandaoni

Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Yobnesh YusuphBatuli’ wamerushiana maneno kupitia akaunti zao kwenye mtandao wa Instagram kufuatia madai aliyoyatoa Batuli kuwa amedhulumiwa na Ray kwenye filamu ya Tajiri Mfupi ambayo batuli ameigiza.

Alianza Batuli kwa kuandika haya;

Haki Ya Mtu Haizami
Swali: Movie Yako Nimecheza Mwaka Juzi Wiki Moja Kabla Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Makubaliano Yetu Ya Kazi Kimkataba Ni Siku 10 Tu Lkn Ulienda Kinyume Na Matokeo Yake Nilifanya Kazi Yako Mwezi Mzima Wa Ramadhan Je Ulikuwa Sawa!? Swali: Pamoja Na Usumbufu Wako Wote Nilifanya Kazi Sikufanya!? Kumbuka Nilikuwa Kwenye Swaumu
Swali: Toka Mwaka Juzi Mpaka Mwaka Jana Ni Mm Ndie Niliekuwa Nafuatilia Malipo Yng Ofisini Sio Chini Ya 20 Times Na Umekuwa Ukinikimbia Matokeo Yake Nikachoka Kuja, Simu Zng Umekuwa Ukizipokea Unapotaka Na Sms Unanijibu Unavyotaka Je Mkataba Wetu Ulisema Hivyo!? Swali : Naimani Ww Una Mkataba Upo Ofisini Kwako Upige Picha Tuone Kama Upo Unavyodai, Binafsi Kila Mtu Anajua Nyumba Yng Iliteketea Moto Hivyo Sina Kitu Na Ndio Maana Umekuwa Ukinitendea Unyama Huu Je Kuna Anaeweza Kukaa Kimya Zaidi Ya Mwaka Mmoja Na Hatimae Unaona Kazi Inatoka Wakati Hujalipwa!?
Swali : Ni Movie Ngapi Nilizofanya Kwenye Kampuni Yako Chini Ya Johari!? Ni Zaidi Ya 3 Je Nililalamika!? Kwanini Hii Ambayo Johari Hakuwepo Nikaingia Mkataba Na Ww Iweje Nilalamike!? Dhulma Itakufikisha Pabaya Sana, Tambua Nilifanya Kazi Yako Ktk Mazingira Magumu, Nilikuwa Kwenye Swaumu Baba Nilifuturu Mabarabarani Chipsi Na Vingine Visivyo Rasmi Yote Ni Ktk Kutimiza Kazi Yako, Nionyeshe Mkataba Unaosema Nilipwe Baada Ya Mwaka 1 Na Kuendelea Hakika Umeonyesha Ulivyo Na Roho Ya Dhulma Sijawahi Kulalamika Popote Kuhusu Unachonifanyia Kwa Sbb Nilijua Ipo Siku Utanilipa Changu Matokeo Yake Umeona Ujivishe Ujemedari Lakini Haitokisaidia Chochote, Kama Haki Yng Basi Itanifuata Hata Nikiwa Kaburini….Be Blessed….Allah Bariq

Ray akajibu kwa kuandika haya;

KATIKA MAISHA YANGU HUWA SIYUMBISHWI WALA SITIKISIKI KWENYE MISIMAMO YANGU NA SIKU ZOTE UKITAKA KUWA MTETEZI MZURI LAZIMA UWEZE KUSIKILIZA PANDE ZOTE MBILI ZA SHILINGI. NINA MIAKA 15 KWENYE TASNIA HII YA FILAMU UKUWAHI KUSIKIA NENO LINALOITWA DHURUMA KUTOKA KWANGU ILA WASWAHILI WANASEMA USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA. NASEMA HIVI NIKIKUPA WALAU UTENGENEZE NUSU FILAMU TU NADHANI HAYA MATUSI YOTE MNAYOTUKANA MNGEGEUKA UPANDE WA PILI WA SHILINGI. JINSI WATU WANAVYOSHINDWA KUESHIMU KAZI ZA WATU COZ WAO WANA NJIA NYINGI ZA KUPATA KIPATO AMBAZO HIZO NJIA SISI HATUWEZI ZIFANYA LAZIMA TUFANYE KAZI ILI MKONO UENDE KINYWANI. MTU YOYOTE ANAYECHEZEA MAISHA YAKO MUOGOPE KAMA UKOMA. ISHU YA BATULI IKO KIMKATABA ZAIDI YA YEYE KAMA UPANDE MMOJAWAPO WA KUTEKELEZA MKATABA ANAJUA ILO. UPANDE MMOJA WA MKATABA UNAPOSHINDWA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE NJIA ZA KUPITA ZIKO WAZI NA ZINAJULIKANA….INAPOFIKIA MTU BADALA YA KUFUATA NJIA SAHIHI NA AKAAMUA KULETA MJADALA KWENYE SOCIAL MEDIA HAPO KUNA ULAKINI AU AMEAMUA KUJIPA UPOFU WA SHERIA YA MIKATABA NINGEPENDA MUHUSIKA AJIKUMBUSHE ILO NA AFUATE NJIA SAHIHI. KUTUMIA SOCIAL MEDIA HAZITAMSAIDIA ZAIDI YA KULIKUZA JAMBO KWA WATU WASIOJUA UNDANI WAKE.

Filamu ya Tajiri Mfupi inatarajia kuingia sokoni hivi karibuni..

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364