Nuh Mziwanda Amwangukia Shilole
STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.
“Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi.
“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana. Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.
“Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi.
“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana.
Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.
Chanzo:GPL