Prof. Elisante Awaasa Wasanii Kuacha haya
Serikali imesema ina nia njema na wasanii na kuwataka kutojihusisha na vitu haramu, kwani sio mfano mzuri kwa jamii wakiwa kama kioo kwao.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo.
“Serikali kwa kweli ina nia njema na iko tayari kushirikiana nao kwa ajili ya kufanya mambo mengi ya kuendeleza jamii, tukisisitiza kwamba wasijiingize kwenye shughuli haramu, wafanye shughuli sahihi na serikali iko pamoja nao, watakapojiingiza kwenye shughuli haramu watakuwa wamechafua ule ukioo wao yani ile hadhi yao inachukua muda jamii”, alisema Prof. Elisante.
Pia Prof. Elisante amesema iwapo wakifanya hivyo ni ngumu kurudisha imani yao kwa wananchi, na kuendelea kuwaheshimu na kuwathamini.
“Mara nyingi kufanya jamii ikuamini inachukua muda kujenga, inachukua zaidi ya miaka 10 kujenga jina lako, lakini kuharibu lile jina lako kama msanii, unahitaji kosa moja tu, ambalo hilo kosa labda la sekunde tatu, ila ukishadhalilika inakuchukua muda mrefu, na mara nyingine haiwezekani kurudisha ile heshima”, alisema Prof. Elisante.
eatv.tv