-->

Sijapenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike – Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa Hip Hop Nay wa Mitego amesema hakupenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike kama baadhi ya mashabiki wa Wema Sepetu wanavyodai katika mitandao ya kijamii.

NAY28

Rapa huyo kupitia wimbo wake “Shika Adabu Yako’ alimchana Wema ‘una mimba kweli, au ndio kiki za msimu?. Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu” kauli ambayo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki wa Wema.

Akizungumza katika kipindi cha Ubaoni cha EFM Jumatano hii, Nay alisema yeye hawezi mwombea mabaya Wema kwa kuwa anapenda sana watoto.

“Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda watoto. Kama ilikuwa mimba kweli nampa pole sana dada yangu ila kama ilikuwa kiki imefika mwisho Kwani nilichoongea kwenye wimbo ilikuwa ni swali Je? Una mimba kweli au drama.,”alisema Nay.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364