-->

Sikumbuki Hata Kukutana na Gigy Money – Mavoko

Msanii Rich Mavoko amekanusha taarifa za kuwahi kuwa na mahusiano na video queen Gigy Money, ambaye alisema alishawahi kuwa naye akiwa kidato cha pili.

Giggy-Money

Akiongea na East Africa Radio Mavoko amesema taarifa hizo si za kweli, na hakumbuki hata kuwahi kukutana naye mrembo huyo, achilia mbali kuwa na mahusiano naye.

“Mi sijawahi kutoka naye, hata siku moja sijawahi, sina urafiki naye na wala sijawahi kuongea naye, sijui kama alishawahi kukutana na mimi, sijaweka kichwani kama nishawahi kukutana nae sikumbuki.

Mavoko ameendelea kusema “Sijawahi kuwa na skendo za kipumbavu, mi ni mtu ambaye sijawahi kuwa na upumbavu kama huo, kwanza mi mwenyewe nashangaa unajua kila kitu, sijawahi kutoka naye sijui mwenyewe anafikiria nini, siwezi kujua, siwezi kutambua, sijawahi kuelewa nini kilichompelekea hivyo”, alisema Richi Mavoko.

Hivi Karibuni video queen huyo alisema alishawahi kuwa na mahusiano na msanii huyo wakati yupo kidato cha pili, kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi na hakifai kwa mtu ambaye ni kioo cha jamii.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364