Ukimya Wangu Umefanya Nijipange Zaidi – Marlaw
Msanii wa bongo fleva Lawrence Malima maarufu kama Marlaw ambaye alitamba na nyimbo nyingi kipindi cha nyuma kama Rita, Missing my baby, Bembeleza na nyinginezo amesema kuwa ukimya wake umempa nafasi nzuri ya kujipanga na kufanya kazi nzuri zaidi.
Marlaw ambaye aliweza kutambulisha style ya kiduku kwa mara ya mwisho alitamba na wimbo wake wa Pii-Pii ambao uliaandaliwa na mtayarishaji Tuddy Thomas na kuweza kubamba katika sehemu mbalimbali za nchi na kuchochea aina ya uchezaji ambao ulifahamika kama kiduku.
Baada ya wimbo huo Marlaw alikuwa kimya kisanaa na baadaye alifunga ndoa na msanii mwenzake wa Bongo fleva Besta.
Lakini Marlaw amewatoa wasiwasi mashabiki zake na kusema kuwa wakati wa ukimya wake kimuziki amepata nafasi nzuri ya kutosha kuandaa kazi zake za sanaa na kusema kuwa baada ya muda mfupi mashabiki wataweza kumsikia na kusikia kazi zake mpya na kuziona pia.
“Ni kweli mimi nipo na nipo vizuri kabisa maana Mungu anasaidia, ukimya wangu ni kwamba umenipa nafasi nzuri kuandaa tu kazi zangu kwa hiyo baada ya muda mfupi mashabiki wategemee kumsikia Marlaw na kuona maana nipo jikoni sasa nafanya mambo kwa ajili ya mashabiki zangu”
eatv.tv