-->

Taarifa kutoka Hospitali aliyopo Wastara kuhusu Matibabu yake


February 10, 2018 imetolewa taarifa na Masoud Kaftany ambaye ni Afisa Habari, Uenezi , Mahusiano katika chama cha Waigizaji Kinondoni, kuhusu Muigizaji Wastara Juma taarifa hiyo inasema Wastara ameshafanyiwa Vipimo (Operation ) na anaendelea kupatiwa Matibabu.

Muigizaji Wastara ambaye yupo katika Hospitali ya Saifee (Mumbai ) Nchini India anaendelea vizuri na siku hiyo ya jana alitembelewa hospitalini na Muigizaji wa Bongomovie REGINA KAOLE ambaye yupo Mumbai nchini India kwa shughuli zake za kikazi.

Wanatasnia na wadau wa filam nchini wanaombwa kuzidi kumuombea Muigizaji huyo Wastara ili apone Haraka na kurejea nchini salama.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364