-->

Waandishi wa ‘Script’wanatuangusha – JB

jb32 (2)

Msanii nguli wa filamu za kitanzania Jacob Steven maarufu kama JB, amesema kushuka kwa thamani kwa filamu za sasa hivi ukitofautisha na zile za zamani, kunasababishwa na waandishi wa hadithi kutofanya vizuri, na upungufu wa waongozaji wazuri.

B ameyasema hayo alipokuwa akiongea na East Africa Television, na kusema kwamba filamu yoyote inatengenezwa na hadithi nzuri inayoandikwa na ‘script writers’, lakini kitendo cha wao kutoiandika ipasavyo na kwa ubunifu, ndiko kunakopoteza ubora wa filamu.

“Kitu chochote kikikaa kwa muda watu wanachoka na watu wanapochoka kunatakiwa kufanya mabadiliko ili kufanya iwe sawa, kuna namna ya kucheza na mashabiki ili kuwafanya wabaki, sinema zote ziliandikwa, waandishi ndiyo wanatengeneza sinema, mwandishi akiwa hana jipya ni tatizo, pia tuna tatizo la directors, sasa jinsi ya kuwapata waandishi wazuri ndiyo tatizo, kwani sanaa kila mtu anatamani kuingia hata kama hana uwezo”, alisema JB.

Pia JB amesema tatizo lingine linaloikabili sekta hiyo ni jinsi mfumo wa uuzaji wake ulivyo, pamoja na jinsi ya kuitangaza biashara hiyo ya filamu na kufika mbali zaidi hadi kimataifa.

“Problem ni namna ambavyo tunazimarket, zamani soko lilikuwa linahitaji filamu, tunavyozimarket filamu ni tatizo, sasa hivi kila filamu inatangazwa, kuna mwingine anatangaza ni mbaya, lakini hivi vyote vitakuwa historia”, alisema muigizaji huyo ambaye anafanya vizuri kwenye filamu za Tanzania.

Pia JB amesema watu wanatakiwa kuondoa dhana kwamba bongo movie inakufa, na badala yake waipende kwani ndio zao la hapa nyumbani.

“Mfano bongo fleva, watu walisema inakufa lakini ndiyo kwanza inakuwa zaidi, bongo movie haitakufa, watakaokufa ni waigizaji, na kisha watakuja wapya na wao wataipeleka mbali, mi naiona bongo movie mpya kabisa tena ya kimataifa, tena we should be proud of bongo movie, hii ni ya kwetu”, alisema JB.

Kwa sasa JB amesema kuna kitu kipo jikoni ambacho kitasaidia kusukuma tasnia ya filamu kiujumla, lakini hawezi kukizungumzia kiundani ni kitu gani hasa mpaka muda muafaka utakapofika.

EATV.TV

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364