-->

Wanaosema Nimefulia ni Mamluki na Kenge -Dudu Baya

Msanii Dudu baya amewalalamikia Watanzania na kusema kuwa hawafikirii kitu kingine cha msingi pale msanii anapokuwa kimya, na badala yake wanakimbilia kusema msanii huyo amefulia.

dudu baya

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Dudu baya amesema mashabiki weni ndio wa kwanza kulaumu kuwa wasanii wa Tanzania hawana elimu, hivyo wakikaa kimya ili kufanya mengine ikiwemo na elimu huwadharau.

“Wanacomplain Dudu baya yuko kimya, wanataka niwaimbie kila siku, na end of the day mashabiki wa Tanzania huwa wanasema wasanii wa Tanzania hawana elimu, lakini msanii anapopotea kwenye game, labda karudi chuo kama alivyuokuwa Crazy GK juzi karudi kagraduate ana masters, lakini watanzania wakishaona msanii yuko kimya basi wanasema amefulia, wakati kuna wengine wapo chuo wengine wanafanya issue zao”, alisema Dudu Baya.

Pamoja na hayo Dudu baya amewajia juu mashabiki wanaosema kuwa amefulia na kumsema anashinda maskani, na kuwaita ni mamluki wametumwa kumuharibia, huku wakimtuhumu kutumia kilevi kwa kupitiliza na kumfanya ashuke kimuziki.

“Nikawasikia wanasema mi nashinda maskani, sifanyi game ya muziki na vitu kama hivyo, walikuwa wanacomplain Dudu baya anakunywa muda wote, what is ur business, mimi natumia kon****, kuna watu wanatumia madawa ya kulevya, ugolo sijui sigara, alafu hawa jamaa dizain wametumwa ni mamluki, hawa ni mamluki kwa sababu kwanza hawanijui vizuri hawajui nini nafanya apart from music, wanaongea ongea tu na mapombe yao na viroba vyao na vitu kama hivyo, unatakiwa uiongee vitu unavyovijua, hawa ni kenge na wataendelea kuwa kenge, mimi ni mamba”, alisema Dudu baya.

eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364