Watanzania Waliomba Majina ya Watumia ‘Unga’ Yatajwe Hadharani-Makonda
Makonda amesema katika uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alipigiwa kelele ili awataje wahusika wa dawa za kulevya lakini aliamua kuacha vyombo vyenye mamlaka vifanye kazi yake.
“Mzee Jakaya mlimpigia kelele…ooh taja taja, taja taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama mlivyokuwa mnataka.”
“Wakaibuka tena, haaa hapana hiyo siyo busara haa…uliona wapi giza linaondolewa kwa kutumia giza? .Aliyefanya mafichoni anawekwa hadharani na harudii tena,”amesema
By Kelvin Matandiko, Mwananchi