Wolper Akanusha Kuihama CHADEMA na Kukataa Kuitwa ‘Jacqueline Lowassa’
Staa mrembo wa Bongo Movies, Jacqueline Woper ambaye alikuwa msatari wa mbele kumpigia kampeni aliekuwa mgombe urasi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye uchaguzi wa mwaka jana, Mh. Edward Lowassa amekanusha habari iliyoripotiwa na moja ya magazeti ‘pendwa’ kuwa kwa sasa staa huyo ameshajitoa CHADEMA na hataki tena kuitwa mtoto wa Lowassa ‘Jacqueline Lowassa’ kama alivyo jiita kipindi kile cha kampeni.
Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Wolper aliweka picha ya gareti hilo na kuandika haya.