Zari amuuliza Diamond “Madale state lodge au guest house?”
Baada ya tetesi kuzidi kuenea katika mitandao ya kijamii na watu kuzidi kusema kuwa inawezekena Tunda ana mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz kutokana tu na ukaribu walionao wawili hao.
Zari the boss lady ambaye ni mzazi mwenzake Diamond Platnumz ameonekana kupata taarifa hizo kuhusiana na tetesi zinazoendelea katika mitandao ya kijamii na kuamua kuandika ujumbe kwa Diamond Platnumz kupitia mtandao wa snapchat.
Maneno hayo aliyoyaandika Zari kupitia mtandao wa snapchat yanasadikika kuwa yanaweza yakawa yanamlenga Diamond Platnumz kutokana na kudaiwa kuwa anapeleka wasichana Madale kila kukicha.