Zari Awajibu Wanaodai Hamkumbuki Ivan
AMEWAJIBU! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz, Zari kutembelea kaburi la aliyekuwa mumewe marehemu Ivan Semwanga ‘Ivan Don’, Kayunga, jijini Kampala, Uganda.
Mrembo huyo ambaye amekuwa akipata wakati mgumu kutoka kwa watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimtuhumu kutomkumbuka mume wake huyo wa zamani, aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, juzi alitumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha kuwa watu huwa wanakosea.
“Watoto waliniomba kuja kusalimia, nikawaambia wasijali, pumzika kwa amani, mapema mno, lakini uko nasi kiroho,” aliandika Zari kwa Kiingereza huku akisindikiza maneno hayo na picha aliyopiga kwenye kaburi la Ivan.
Mtanzania