-->

Zari, Mama Diamond Watifuana Mbele ya Wazungu

Inadaiwa ilitokea lakini haikuandikwa! Kuna habari kuwa, ile safari ya familia ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kula bata kwenye nchi za Ulaya, ilikuwa na mambo mengi lakini kubwa ni madai ya kuwepo kwa mtifuano kati ya mama Diamond, Sanura Kasim na Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenzake, Diamond.

ZARI NA MAMA DIAMOND

Kwa mujibu wa chanzo, mtifuano kati ya Zari na mkwewe huyo ulitokea baada ya siku moja mkwe huyo kuteleza kwenye ngazi za umeme wakiwa wanapanda, Zari akamuwahi kwa kumshika mkono hali iliyomtibua mama huyo.

“Jamani kuna hili la mama D (Diamond) na Zari kutibuana nchini Sweden. Wakiwa kule, siku moja walikuwa wakipanda zile ngazi za umeme, sasa mama Diamond akateleza, Zari akasema amuwahi ili mkwewe asifike chini, si akamchenjia. Aliusukuma mkono wa Zari na kumwambia amwache mwenyewe.

“Naamini kuna kutokuelewana kwa ukweli kabisa kati ya mama Diamond, bintiye yule Esma dhidi ya Zari.
Wengi wanasema Zari anataka kutawala, mama Diamond hataki kutawaliwa.

“Na kuhusu hili la Zari na ndugu wa ukweni kwake kutoelewana, Diamond asimame kama mwanaume liishe. Kama mama na Zari hawaivi aamue moja. Lakini siyo mbele za watu wanasema wanaiva, ndani hawaivi. Si sawasawa,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya madai hayo, gazeti hili lilimpigia simu mama Diamond na kumsomea mashitaka yake ambapo baada ya kusikiliza mpaka mwisho, alisema:
“Mimi na Zari hatuna ugomvi we’ nenda kamuulize vizuri huyohuyo aliyekuletea umbeya huo,” (akakata simu). Alipopigiwa tena hakupokea.
Pia, Amani lilimsaka Esma na kumuuliza kuhusu madai ya Zari kutoiva na familia.
“Pengine unazungumzia maneno niliyoyaposti kwenye mtandao (hakuyafafanua). Mimi nikisema mtu simlengi Zari japokuwa ni kweli hatuko naye poa kivile. Mimi huwa nawalenga wengine,” alisema Esma.
Diamond alikosekana hewani, lakini siku za nyuma aliwahi kusema kuna watu wanasemasema sana kuhusu Zari na mama yake, ila yeye hawezi kuwazuia kusema kwa vile midomo ni mali yao.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364