-->

Sikutaka Hela ya Mtu – Wastara

Msanii wa filamu wa bongo Wastara Juma ambaye hivi karibuni amepewa mchango wa milioni 15 na familia ya Rais Magufuli, amewajibu watu wanamtuhumu kuwa tapeli kwani hana ugonjwa unaomsumbua.

Akizungumza na mwandishi wa EATV Wastara amesema kabla ya kuomba michango alijitahidi sana kujitafutia mwenyewe hiyo pesa kwani hakutaka pesa ya mtu mwengine ije imsaidie, kwani alijiona anakuwa mzigo kwa jamii.

Kufuatia kauli hiyo Wastara amesema alishajaribu kujiingiza kwenye biashara ambazo amedai hazina faida, mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuza vitu vya ndani, jambo ambalo msanii mwenzake Steve Nyerere alimkataza, na kumshauri aweke wazi matatizo yake iili watu wamsaidie.

Akiendelea kulalamikia kitendo cha watu kumdhihaki, amesema asilimia kubwa ya watu wanaomtuhumu hawajahi hata kwenda kumuona wakiwemo wasanii wenzake, ambao waliamua kumtenga baada ya yeye kuolewa na aliyekuwa Mbunge wa CCM Sadifa.

Msikilize hapa

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364