-->

Category Archives: Bongomovies

artists from Tanzania , East AFRICA

Muhogo Mchungu: Jamani Mimi Sijafa wala Siu...

Post Image

Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Abdallah Makumbila alimaarufu kama Muhogo Mchungu amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki na kusema kuwa yeye saizi hasumbuliwi hata na mafua. Muhogo Mchungu alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Supamix cha East Africa Radio amesema kuwa kwa sasa anafanya utaratibu wa kwenda kumshtaki mtu ambaye amesambaza […]

Read More..

Wastara Apata Ubalozi wa Simu za KZG, Atali...

Post Image

Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa Kampuni ya simu ya mkononi ya KZG ambapo leo amekabidhiwa na kusainishwa mkataba rasmi. Akizungumza katika tukio la kusaini makubaliano ya kuwa balozi wa kampuni hiyo  lililofanyika katika ukumbi wa De Mag Hotel iliyopo Mwananyamala, Dar,  Wastara alisema amefurahi sana kupata shavu hilo […]

Read More..

Barafu Aiponda Biashara ya Bongo Movie

Post Image

Msanii wa Bongo Movie Barafu amesema biashara ya movie ni kama biashara kichaa kwa kuwa inamlazimu msanii kufanya kazi na kuipeleka kwa “Mhindi” ambaye hadi auze kwanza arudishe pesa ndipo amlipe msanii. Akiongea na eNewz Barafu amesema “biashara ya move ni tofauti na mtu anayeuza pipi au duka kwa kuwa unatengeneza movie kwa mamilioni lakini […]

Read More..

Aunt Ezekiel Awajibu Wanaodai Anajipendekez...

Post Image

Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Aunt Ezekiel amewamind mashabiki katika mitandao ya kijamii ambao wanadai anajipendekeza kwa mama watoto wa Diamond, Zari, baada ya hivi karibuni kuonekana akila nao bata pamoja. Mwingizaji huyo ambaye alikuwa rafiki wa Wema Sepetu, amesema lazima awe karibu na familia ya bosi wa mume wake kwa kuwa […]

Read More..

Makonda Awashukuru Mastaa Wanaoiunga Mkono ...

Post Image

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa shukrani kwa muigizaji Jacqueline Wolper na wengine wanaoiunga mkono kampeni yake ijayo, Mti Wangu. Mkuu wa mkoa huyo ametoa shukrani zake katika ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha ya muigizaji akiwa amevaa t-shirt yenye logo ya neno ‘mti wangu’ akionesha juhudi za kumuunga mkono. […]

Read More..

Ukibana Ndani Nje Tunatoboa- Barafu

Post Image

MWIGIZAJI wa filamu Swahilihood Suleiman Barafu amesema kuwa wakati kuna wakati wa filamu nchini hawatoi nafasi kwa waigizaji wenye uwezo kama yeye watayarishaji wa filamu wa nje wanawaona na kuwaita kwa ajili ya kushiriki katika kazi zao, na anafanya kazi nchini Kenya. “Nashukru Mungu kazi yangu ya uigizaji imefika mbali kwani kama inafikia mtayarishaji kutoka […]

Read More..

Pastor Myamba: Waigizaji Ndio Wanaua Soko l...

Post Image

Muigizaji mahiri wa filamu Bongo, Emmanuel Myamba maarufu kwa jina la Pastor Myamba ameitaja sababu ya kushuka kwa soko la filamu nchini kuwa ni kutokana na wasanii wenyewe. Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha Ulimwengu wa Filamu cha TBC 1 kuwa wasanii wamekuwa wakipunguza juhudi za kutengeneza sinema nzuri kwa ajili ya kupunguza gharama. “Kama watu […]

Read More..

JB Kuzalisha Waigizaji Wapya

Post Image

Msanii wa filamu nchini Jacob Steven (JB) amefunguka na kusema kuwa kuna wasanii wengi wachanga ni wazuri katika tasnia ya filamu nchini lakini hawapewi nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kuigiza ndiyo maana tasnia hiyo imekuwa na wasanii walewale. Akiongea kwenye kipindi cha 5Selekt, Jacob Steven (JB) alisema kwa sasa kupitia kampuni yake ya Jerusalem […]

Read More..

Nay Wa Mitego Aitakia Mema Ndoa ya Shamsa F...

Post Image

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameitabiria mema ndoa ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Shamsa Ford. Shamsa ambaye alikuwa mpenzi wa rapper huyo alifunga ndoa mwezi mmoja uliopita na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi. Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay Wa Mitego amesema Shamsa […]

Read More..

Senga Awaponda Wachekeshaji wa Bongo

Post Image

Msanii mkongwe wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la Senga, amepiga stori na eNewz na kufunguka kuhusu sanaa ya vichekesho nchini na kusema kuwa Bongo kwa sasa wachekeshaji ni wachache sana, na kwamba wengi ni waigizaji. Senga alisema wengi wanaojita wachekeshaji kwa sasa ni watu ambao si comedians, bali ni waigizaji wa kawaida wanaolazimisha tu […]

Read More..

Kalambati lobo ya JB Kuonyeshwa Leo Sibuka ...

Post Image

Zikiwa zimebaki saa chache tu wapenzi wa filamu za kitanzania kushuhudia kwa mara ya kwanza filamu kubwa ya Kalambati lobo,kutoka kwa msanii grade 1 bongo movie JB ikioneshwa kwenye channel bora ya filamu Tanzania Sibuka Maisha channel namba 111 kwenye startimes leo saa 3 usiku. Tumewasogezea picha za Jb akila dinner na washindi walioshindwa swali […]

Read More..

JB Aongea Kuhusu Mfumo Huu Mpya wa Uzinduzi...

Post Image

Mcheza filamu maarufu Jacob stephen (JB) amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutambulisha mfumo mpya wa kuonesha filamu kupitia media ya Sibuka Maisha channel 111 kwenye startimes kabla ya kuingia madukani. Amesema filamu hiyo inaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa tarehe 23 mwezi huu saa 3 usiku na kurudiwa Jumamosi na Jumapili […]

Read More..

Mrembo Nakufa Kwa Ukimwi, Amtumia Ujumbe Au...

Post Image

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni muumini wa kanisa mojawapo jijini Dar, anayeshirikiana na wenzake kufanya maombi nyumba hadi nyumba, wamekutana na mrembo aliyekataa kumtaja jina maeneo ya Kawe, akiwa hoi akidai anakufa kwa Ukimwi, lakini akataka wafikishe ujumbe wake kwa msanii wa filamu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’. Akizungumza kwa njia ya simu aliyopiga chumba chetu […]

Read More..

Bongo Movie Haijafa- Batuli

Post Image

KUNA wakati ambapo kila mtu huwa na lake la kusema katika kuongelea jambo linalogusa maslahi yake kama mwanadada msanii mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ anayepingana na kauli ambazo hutolewa na baadhi ya wasanii kuwa tasnia ya filamu imeshuka au inaelekea kaburini. “Huwezi kubishana na mtu kuhusu kusema kuwa Bongo Movie imeshuka […]

Read More..

Wema Awapa Makavu ‘Team Wema’

Post Image

Muigizaji nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amewatimua watu wanaojiita Team Wema waliotapakaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, akisema hawataki kwa vile wanamharibia maisha yake. Katika sauti aliyoituma katika akaunti ya mtandao wake wa Instagram, alisema haelewi hasa asili ya watu hao kujihusisha na jina lake, lakini anakerwa zaidi nao kwa kitendo chao cha kutaka […]

Read More..

Rose Ndauka Kuwa Mtangazaji wa Runinga

Post Image

Malkia wa filamu, Rose Ndauka atakuwa mtangazaji wa kipindi kipya cha runinga kiitwacho ‘SK TV Show’. Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, atakuwa akitangaza kipindi hicho cha runinga akiwa na Fahad Fuad. SK TV Show ni kipindi ambacho kitakuwa kinatoa habari mbalimbali pamoja na matukio yanayotokea katika jamii. Hata hivyo mwigizaji huyo hakuweka […]

Read More..

Lulu: Sasa Nahitaji Kupata Mtoto

Post Image

Staa mrembo wa Bongo Movie amefunguka kuwa kwasasa anahitaji kuwa na mtoto. Muigizaji huyo ameandika ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram akimuomba Mungu huku akidai kuwa yupo tayari kwa sasa na anahitaji mtoto. “Okay…I’m ready noooow????and I want a Baby Boy???In Jesus Name?,” ameandika Lulu kwenye mtandao huo. Kwa sasa muigizaji huyo yupo kwenye mahusiano […]

Read More..

Lungi Maulanga, Achezea Kichapo ‘Hevi’ ...

Post Image

Muigizaji wa kitambo Bongo, Lungi Maulanga, anadaiwa kuchezea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa mpenzi wake wa zamani (jina linahifadhiwa), kisa kikiwa ni kumnyima unyumba baada ya kukutana baa na kumtaka waondoke pamoja. Chanzo makini ambacho kilishuhudia mtiti huo kilidai kwamba, Lungi, akiwa anapata kinywaji kwenye baa moja maeneo ya Kinondoni, jamaa huyo aliibuka ‘from no where’ […]

Read More..